IMF AFRITAC East reposted this
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East, iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linaendesha program ya kuongeza ujuzi katika baadhi ya nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Eritri na Malawi. Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka.
-
-
-
-
-
+3